Home Soka Ihefu Yatimua C.E.O

Ihefu Yatimua C.E.O

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa klabu ya Ihefu Sc umefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha Mkataba wa kazi na aliyekua Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Biko Mangasini Scanda ikiwa takribani siku arobaini na tatu tangu imtangaze kujiunga na timu hiyo Novemba 22 mwaka jana.

Katika taarifa yake kwa umma uongozi wa timu hiyo umemshukuru Biko kwa utendaji wake chanya ndani ya timu yetu kwa muda aliokua nao na bado una thamini na kupongeza kazi alizofanya klabuni hapo kwa kipindi kifupi alichohudumu.

Ihefu Fc imekua na mapito magumu msimu huu ikianza kuondokewa na kocha Zubeiry Katwila kisha ikamuajiri kocha Moses Basena ambaye naye ameondolewa kutokana na matokeo mabovu na sasa ni zamu ya Mtendaji mkuu ambaye naye ameondolewa ikiwa na njia ya klabu hiyo kurudisha ufalme wake katika ligi kuu nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited