Beki wa klabu ya Simba Mganda Juuko Murshid ameweka ngumu kuripoti klabuni kujiunga na timu katika kambi ya maandalizi ya msimu akishinikiza kuachwa ajiunge na timu nyingine.
Mchezaji huyo aliyeiongoza Uganda katika michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2019) yanayofanyika nchini Misri imedaiwa kuwa hana mpango wa kuendelea na klabu hiyo hivyo anashinikizwa kuachwa ili atafute timu nyingine ingali bado ana mkataba na mabingwa hao mara mbili mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Akizungumza na Wanahabari Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Crescentius Magori alithibitisha kukata mishahara ya mchezaji huyo kama adhabu ya utoro aliyoionyesha klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Juuko 26 alisajiliwa na Simba misimu kadhaa iliyopita licha ya kujihakikishia namba katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda(The cranes) amekua na wakati wa kusuasua katika klabu ya simba kutokana na matatizo ya kinidhamu likiwemo suala la utoro.