Mshambuliaji wa klabu ya Simba Meddie Kagere ametua nchini huku akitamba kuwa amekuja kumalizia kazi aliyoianza ya kuhakikisha anakua mfungaji bora wa ligi kuu nchini na kubeba kiatu cha dhahabu.
Staa huyo matata ametua nchini akitokea nchini Rwanda alipokua baaada ya ligi kuu kusimamishwa kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Corona.
Mastaa mbalimbali wa klabu ya Simba walikua nchini isipokua Kagere,Cletous Chama na Eldin Shiboub waliokua nchini mwao hivyo sasa klabu hiyo inajiandaa kuwapokea Chama na Shiboub ili kukamilisha kikosi cha kinachotarajiwa kuanza mazoezi wiki hii.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.