Home Soka Kahata Atimka Simba sc

Kahata Atimka Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mchezeshaji wa Simba raia wa Kenya, Francis Kahata ameshindwa kufikia muafaka mzuri na timu yake katika dau la usajili huku akikwea pipa kurejea nyumbani kwao nchini Kenya.
Kiungo huyo juzi rasmi alimaliza mkataba wake wa miaka miwili ya kukipiga Simba aliyojiunga nayo msimu wa 2019/2020 akitokea Gor Mahia ya nchini Kenya kama mchezaji huru.
Nyota huyo hivi karibuni jina lake lilikatwa katika usajili wa Ligi Kuu Bara na nafasi yake kuchukuliwa na Mzimbabwe Perfect Chikwende aliyejiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa Simba imeshindwa kufikia muafaka mzuri wa kumuongezea mkataba baada ya kushindwana katika maslahi kwenye pande hizo mbili huku taarifa zinasema kuwa uongozi wa Simba ulimpa mkataba aliotakiwa kusaini bure huku wakiboresha mshahara wake wa kila mwezi pekee, kitendo ambacho amekikataa kiungo huyo kabla ya juzi jioni kukwea pipa kurejea kwao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited