Ni kama hana bahati kwani licha ya kushindwa kucheza mara kadhaa kutokana na kuandamwa na majeraha straika Mzambia wa Yanga Mybin Kalengo amevunjika mguu na kulazimika kupelekwa hospitali haraka.
Nyota ambaye yuko katika kambi ya klabu hiyo jijini Mwanza wakijiandaa na mchezo dhidi ya Pyramids fc ya Misri aliumia wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba ya jijini Mwanza na kulazimika kukimbizwa hospitali ya Bugando jijini humo.
Staa huyo kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo yuko njiani kuja Dar ili kupatiwa matibabu katika hospitali ya muhimbili na ataukosa mchezo huo gumzo nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.