Home Soka Kessy Huru Kuivaa Senegal

Kessy Huru Kuivaa Senegal

by Sports Leo
0 comments

Beki wa Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa stars) Hassan Kessy yupo huru kucheza mchezo wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2019) ambapo Stars itachuana na Senegal siku ya jumapili tarehe 23 mwezi huu baada ya shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kutoa ruhusa ya mchezaji huyo kutumika.

Beki huyo wa zamani wa Mtibwa,Simba na Yanga anayekipiga katika klabu ya Nkana Fc ya Zambia yupo huru baada ya shirikisho la soka la Tanzania (Tff) kuomba ufafanunu kwa Caf kuhusu idadi ya kadi alizotuhumiwa kuwa nazo mchezaji huyo na baada ya Caf kutoa ufafanuzi imethibitisha kuwa mchezaji huyo hana kadi tatu za njano kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Kessy ni mchezaji muhimu kwa timu ya taifa kutokana na kupandisha kiwango  chake hasa baada ya kujiunga na klabu ya Nkana ya Zambia ambapo ameweza kupata uzoefu wa kutosha wa kukabiliana na washambualiaji mbalimbali wakorofi.

banner

Ikumbukwe katika pambano hilo senegali itamkosa mshambuliaji hatari wa Liverpool ya Uingireza Sadio Mane ambaye ana kadi tatu za njano.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited