Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Yanga na Simba Hamisi Kiiza ‘Diego’ yuko mbioni kutua nchini kujiunga na watengeneza sukari Kagera Sugar kwenye dirisha hili dogo la usajili.
Mchezaji huyo aliwahi kufanya vizuri nchini katika klabu ya Yanga na kufanikiwa kutwaa mataji ya ligi kuu soka nchini pia atakumbukwa kwa mchango wake katika kupachika mabao kulikoiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) mwaka 2014 kwa kufunga mabao 5 kwenye michuano hiyo.
Kiiza alihudumu Yanga kuanzia mwaka 2011 hadi mwak 2015 kabla ya kujiunga na wapinzani wao wa jadi Simba mwaka 2015 hadi 2016.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kagera wanashikilia mkia kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC huku tatizo kubwa likiwa ni kushindwa kufunga magoli ya kutosha kufuatia kuondoka kwa washambuliaji wake Vitalis Mayanja na Yusuph Mhilu waliokuwa tegemezi.