Home Soka Kina Samatta Washinda 2-0

Kina Samatta Washinda 2-0

by Dennis Msotwa
0 comments

Mshambuliaji mtanzania Mbwana Samatta ameisaidia klabu ya Aston Villa kuibuka na ushindi wa mbao 2-0 dhidi ya Crystal Palace mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Mahmoud Hassan Trezeguet alikua kinara katika mchezo huo baada ya kupachika mabao mawili yaliyoipa ushindi Aston Villa dakika ya 45+4 na bao la pili alifunga dakika ya 59 na kujipooza machungu ya kufungwa tatu nunge na Manchester United wiki hii.

Aston Villa bado wana hatari ya kushuka daraja licha ya kufanikiwa kushika nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu huku wakitarajiwa kupambana na Everton katika mchezo ujao.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited