Home Soka Kipa Mtibwa atua Yanga

Kipa Mtibwa atua Yanga

by Dennis Msotwa
0 comments

Aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa wakata miwa kutoka Turiani Morogoro Aboutwalib Mshery amejiunga na mabingwa wa kihistoria nchini klabu ya soka ya Yanga hii leo.

Mshery amesaini kandarasi ya miaka miwili na nusu kuwatumikia Wananchi katika michuano mbalimbali inayoshiriki hadi msimu wa 2023/2024.

Kinda huyo anaenda kuchukua nafasi ya mlinda mlango namba moja wa timu hiyo Mmali Djigui Diarra anayekwenda kushiriki michuano ya kombe la Mataifa Afrika(AFCON) itakayoanza nchini Cameroon kuanzia Januari 9 mwakani.

banner

Uwezo mzuri wa kuokoa mashuti makali pamoja na umahiri mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kwa kutumia miguu yake ndizo sifa kubwa zilizompa nafasi ya kusajiliwa Yanga akiwapiku walinda mlango wengine Mbwana Makaka wa Ruvu shooting na Musa Mbissa wa Coastal union ambao nao walikuwa wanahusishwa kusajiliwa Jangwani.

Uzoefu aliopata Mtibwa Sugar ndani ya misimu mitatu ya ligi kuu soka Tanzania Bara ni vitu ambavyo vinamfanya awe tayari kuitumikia timu kubwa kama Yanga.Kipa huyo ataenda kuungana na marafiki zake wa zamani Kibwana Shomari na Dickson Job aliowahi kucheza nao Mtibwa na ambao wamekuwa wakicheza kikosi cha kwanza licha ya ushindani wa namba na majina makubwa ndani ya kikosi cha Yanga.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited