Kitendo cha kurejea kwa baadhi ya Mastaa wa Klabu ya Simba sc waliokua nje ya nchi huku pia kocha wa timu ya Azam fc Aristica Cioaba kimemkasirisha kocha wa Yanga sc Luc Eymael kiasi cha kuposti maneno makali kwa uongozi wa klabu hiyo.
Kocha amesema hajafurahishwa na majibu anayopewa na viongozi wa klabu hiyo kuwa ndege zimejaa baada ya baadhi ya nchi kuruhusu safari za ndege ilihali washindani wake Simba sc na Azam fc zimefanikiwa kuwasafirisha mastaa wao.
Kocha huyo aliyekwama nchini Ubelgiji alisema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akilaumu suala hilo huku timu ikiwa imeanza mazoezi chini ya kocha msaidizi Bonifasi Mkwasa kwa kufuata maelekezo ya kocha huyo aliyeko nje.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Licha ya juhudi za kuwatafuta viongozi wa Yanga sc wazungumzie suala hilo bado ilituwia vigumu kuwapata.