Timu ya soka ya Yanga imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kmc baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Yanga iliandika bao dakika ya Mrisho Ngassa dakika ya 73 akimalizia kazi nzuri ya Patrick Sibomana na Kmc walisawazisha dakika ya 90+4 kwa tuta baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Salum Kabunda na Mwamuzi Henry Sasi kuweka penati iliyofungwa na Abdul Hilary.
Hii ni mara ya kwanza kwa KMC kugawana pointi mbele ya Yanga kwani msimu uliopita ilifungwa nje ndani na kuacha pointi sita kwa Yanga kwenye mechi zilizochezwa uwanja wa Taifa.