Klabu ya Kmc Fc imefanikiwa kuinasa saini ya winga Peter Banda raia wa Malawi na kuizidi kete klabu ya Singida Fountain Gate Fc ambayo ilianza mazungumzo na staa huyo mapema tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Banda ametua Kmc baada ya Singida Fg kuchelewa kukamilisha dili hilo huku kifungo cha kuzuiwa kusajili na Fifa pamoja na TFF kikiwaponza kutokana na kushindwa kulipa fedha kwa wakati ili waepuke zuio hilo.
Banda mchezaji wa zamani wa Simba sc anakwenda Kmc kuiongezea nguvu klabu hiyo hasa katika eneo la ushambuliaji lililochini ya Waziri Junior huku timu hiyo mpaka ligi inasimama ikiwa katika nafasi ya nne ikiwa na alama 21 baada ya kucheza michezo 14 ya ligi kuu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kmc imepanda viwango chini ya mwalimu Abduhamid Moalin kiasi cha kufanya vizuri msimu huu tofauti na msimu ulioisha.