Timu ya soka ya taifa ya wanawake Kilimanjaro Queens imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya chalenji baada ya kuwafunga Uganda katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika uwanja wa chamazi jijini Dar es salaam.
Iliwalazimu mashabiki kusubiri mpaka dakika ya tisini kujua hatma ya mchezo huo baada ya Asha Rashidi “Mwalala” kufunga bao kwa shuti kali akipokea pasi ya Mwanahamisi Omary “Gaucho”.
Kilimanjaro queens itaungana na Kenya kucheza fainali siku ya jumatatu huku Uganda itakutana na Burundi kuwania mshindi wa tatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.