Kocha wa klabu ya Simba Sven Vandebroek amesema bado anamhitaji kiungo Said Ndemla katika klabu hiyo licha ya kumuweka benchi katika michezo mbalimbali.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ambapo alisema “Ndemla ni mchezaji mzuri anayetumia mguu wa kulia huku akipiga pasi ndefu na fupi zinazofika japo anabanwa na changamoto ya kutokua na nguvu”.
Kocha huyo alisisitiza kumhitaji Ndemla kwa kua kila anahitaji kila eneo liwe na wachezaji bora huku akifurahishwa na hatua ya kiungo huyo kutoshuka kiwango licha ya kukaa benchi mara kwa mara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.