Home Soka Kushangilia Kwawaponza Kibu,Diarra

Kushangilia Kwawaponza Kibu,Diarra

by Sports Leo
0 comments

Mastaa Djigui Diarra,Kibu Dennis na Henock Inonga wamepigwa faini na bodi ya ligi kuu nchini kwa kosa la kushangilia vibaya wakati wa mchezo wa ligi kuu baina ya Yanga sc na Simba sc uliopigwa katika uwanja wa Taifa siku ya Novemba 5 mwaka huu.

Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi imewatoza faini ya Tsh. Laki tano (500,000) Wachezaji wa Simba Sc, Kibu Denis na Henock Inonga pamoja na golikipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra kwa makosa tofauti waliyoyafanya wakati wakishangilia magoli yaliyofungwa kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba Sc dhidi ya Yanga SC.

Kibu Denis ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao lake mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga huku akionyesha ishara ya kuwafunga midomo wakati Inonga yeye ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao mbele ya Maafisa wa Benchi la Ufundi la Yanga Sc.

Pia kwa upande wa golikipa wa Yanga Djigui Diarra ametozwa faini hiyo kwa kosa la kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la klabu ya Simba mara baada ya timu yake kufunga moja ya mabao katika mchezo huo wa Kariakoo Derby ambao Yanga sc ilishinda kwa mabao 5-1.

 

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited