Timu ya Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Norwich City katika mchezo wa kufungua pazia la ligi kuu ya uingereza siku ya jana usiku katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Anfield nyumbani kwa majogoo hao.
Katika mchezo huo liva waliweka rekodi ya kufunga mabao mengi katika kipindi cha kwanza kupitia magoli ya Mo salah,Virgil Van Dijk na Divork Origi na huku goli la kujifunga la Grant Hanley lilikamilisha kalamu hiyo ya magoli manne kwa majogoo huku wageni wakipata goli kupitia kwa Teemu Pikki.
Liverpool kwa ushindi huo wanajitengenezea nafasi nzuri ya kukaa kileleni kutokana na kukusanya mtaji mkubwa wa magoli.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.