Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ubelgiji na Chelsea Romelu Lukaku hatimaye amemaliza tofauti zake na kocha mkuu wa timu hiyo Thomas Tuchel kwa kuomba msamaha na kurudishwa kikosini.
Mchezaji huyo aliondolewa kwenye kikosi kilichocheza na Liverpool kutokana na kuvuja kwa mahojiano yake na kituo cha skysports iliwekwa wazi kuwa mchezaji huyo hana furaha na hafurahishwa na jinsi kocha wake anavyomtumia katika kikosi hicho cha mabingwa wa kombe la klabu bingwa Ulaya.
Kocha Tuchel alisema kuwa aliamua kumuweka nje Lukaku ili kutokuchafua hali ya hewa ndani ya timu hiyo na kuwa makelele yaliyotokea kutoka kwenye vyombo vya habari hayakuwa na afya ndani ya kikosi chao.
Baada ya hapo mshambuliaji huyo alianza kuhusishwa na kuondoka ndani ya timu hiyo kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Lakini baada ya kikao cha mwalimu na mchezaji pamoja na maamuzi ya bodi wameamua kuwa mchezaji huyo ataendela kusalia na wala hawana mpango wa kumuuza.