Home Soka Lusajo,Ame Watua Mashujaa Fc

Lusajo,Ame Watua Mashujaa Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Mashujaa Fc ya mkoani Kigoma imekamilisha usajili wa mastaa wawili wa nguvu Ibrahim Ame na Reliants Lusajo kuja kuongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo kilichopo mkiani mwa msimamo wa ligi kuu nchini.

Mashujaa Fc iliyopanda daraja msimu huu imekua na matokeo yasiyoridhisha baada ya kuanza vizuri msimu katika mechi za awali ambapo baadae walipoteza michezo mingi kiasi cha kufunga mwaka wakiwa na alama tisa katika michezo kumi na mbili ya ligi kuu nchini.

Usajili wa Lusajo aliyekua Namungo Fc unakwenda kumaliza tatizo la ufungaji klabuni hapo ambapo mpaka sasa imefungwa magoli mengi kuliko iliyoshinda huku pia ikimsajili Ibrahim Ame kutibu tatizo la ulinzi klabuni hapo.

banner

Mastaa hao mpaka sasa haijawekwa wazi urefu wa mikataba waliyosaini kuitumikia timu hiyo inayomilikiwa na jeshi la ulinzi nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited