Wakati kikosi cha Yanga sc kikiwa tayari kimewasili mkoani Kagera kuivaa Kagera Sugar Fc mastaa wawili wa timu hiyo wanatarajiwa kuukosa mchezo huo utakaofanyika siku ya kesho Ijumaa kuanzia saa kumi jioni katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.
Mastaa hao ni mabeki Ibrahim Hamad na Bakari Mwamnyeto ambao hawajasafiri na kikosi hicho kutokana na kukabiliwa na majeraha waliyoyapata katika michuano ya Afcon wakiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Sambamba na mastaa hao ambao wamekumbwa na majeraha hayo pia Stephane Aziz ki pamoja na kipa Djigui Diarra nao wataukosa mchezo huo kutokana na majukumu hayo ya timu za taifa ambapo Mali imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali huku Burkina Faso yenyewe ikiwa imetolewa nje ya michuano hiyo japo Aziz Ki bado hajawasili nchini.
Mpaka sasa Yanga sc ipo nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 31 baada ya kucheza michezo 11 ya ligi kuu huku Kagera sugar ikiwa nafasi ya 13 na alama 13 za ligi kuu ya Nbc.