Klabu ya soka ya Mamelod Sundowns imefanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa taji la African Football League ikiwa ni mara ya kwanza michuano hiyo kufanyika baada ya kuifunga Wydad Athletic Club kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali wa pili uliofanyika nchini Afrika ya kusini.
Katika mchezo wa kwanza nchini Morroco Mamelod ilikubali kipigo cha mabao 2-1 hivyo kuwalazimu kushinda katika mchezo wa fainali ya pili ambapo walihitaji ushindi wa aina yeyote ili kufuzu na hatimaye mabao mawili ya Peter Shalulile dakika ya 45′ na Aubrey Modiba dakika ya 53′ yalitosha kuipa ushindi Mamelod katika michuano hiyo mipya.
Katika mchezo huo wa Fainali uliofanyika katika uwanja wa Loftus Versfeld Rais wa Fifa Gian Infantino na Rais wa Caf Patrice Motsepe walihudhuria sambamba na viongozi wa timu nane zilizoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa upande wa tuo binafsi kipa wa Mamelod Sundowns Ronwens Williams alitwaa tuzo ya kipa bora huku Taphelo Maseko akitwa tuzo ya mchezaji bora sambamba na mfungaji bora huku tuzo ya mashabiki bora ikienda kwa mashabiki wa klabu ya Simba sc.