Baada ya kupitia kipindi kigumu katika michezo mbalimbali ya ligi kuu nchini Uingereza hatimaye klabu ya Manchester United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Villareal inayonolewa na kocha Unai Emiry katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa barani ulaya.
United inayonolewa na kocha wa muda Michael Carrick haina budi kumshukuru Kipa David De Gea ambaye aliokoa hatari kadhaa langoni kutokana na safu ya ulinzi ya Manchester United kujichanganya mara kwa mara.
Kuingia kwa Bruno Fernandes aliyechukua nafasi ya Donny Van de Beek kuliongeza spidi ya kukaba kuanzia mbele na kuipa presha safu ya ulinzi ya Villareal na kufanikiwa kupata bao la kuongozwa lililofungwa na Cristiano Ronaldo 78′ huku Jadon Sancho akifunga bao lake la pili dakika ya 89′ na kuipa ushindi United huku ikifanikiwa kuongoza kundi hilo baada ya kufikisha alama 10.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.