Klabu ya Manchester United i8mefanikiwa kupata ushindi wa kibabe sana katika moja ya mechi ngumu kwenye Kombe la FA baada ya kuifunga Liverpool Fc kwa mabao 4-3 katika mchezo uliochezwa kwa dakika 90 na 30mza nyongezauliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.
Man Utd chini ya kocha mdachi Erik ten Hag ilianza kupata bao mapema kupitia kwa Scott McTominay dakika ya 10 ya mchezo huku Liverpool ikafunga mara mbili ndani ya dakika tatu za 44 na 45+2 na kuongoza 2-1 kabla ya mapumziko.
Wengi wakiamini kuwa Man Utd itapoteza mchezo huo, Mbrazili Antony alirudisha matumaini baada ya kusawazisha na kufanya matokeo yawe 2-2 dakika ya 87 ya mchezo na kulazimisha mechi hiyo kuingia kwenye dakika 30 za nyongeza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kukosekana kwa umakini kwa Man utd kulisababisha Harvey Elliott kujifungia bao jingine Liverpool dakika ya 105 lakini Man utd walisawazisha kupitia kwa Marcus Rashford dakika ya 112 huku Amad Diallo kufunga bao la nne kwenye dakika 120 na hivyo Man United kupinga nusu fainali ya Kombe la FA kibabe.