Home Soka Man Utd Yakaribia Kumpata Mrithi wa Solskjaer

Man Utd Yakaribia Kumpata Mrithi wa Solskjaer

by Sports Leo
0 comments

Wiki moja baada ya kutimuliwa kwa kocha Olle Gunnar Solskjaer katika klabu ya Manchester United tayari uongozi wa klabu hiyo tajiri upo katika hatua za mwisho kumalizana na kocha Ralf Rangnick mwenye asili ya Ujerumani ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Lokomotiv Moscow ya nchini Urusi.

Kocha mwenye miaka 63 anatarajiwa kupewa nafasi ya ukocha wa muda wa miezi sita huku kukiwa na kipengele cha kuongeza miaka miwili ama kuwa mkurugenzi wa ufundi klabuni hapo.

Rangnick ni muumini wa mpira wa kasi na pasi za uhakika huku akipenda timu yake ikabe kuanzia juu hali inayomlazimu mpinzani kufanya makosa ya mara kwa mara soka ambalo kwa sasa linachezwa na Liverpool ya Jurgen Klopp na Chelsea ya Thomas Tuchel ambao wote wamepitia mikononi mwake.

banner

Tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2012 klabu ya Manchester united imekua na misukosuko ikishindwa kukaa na walimu tofautitofauti huku pia ikiwa na uhaba mkubwa wa mataji kama vile taji la ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited