Ni kama wana ugonjwa mmoja baada ya wote kuambulia sare katika michezo ya ligi kuu nchini Uingereza na kuzidi kudidimiza matumaini ya kumaliza katika nafasi ya nne bora.
United ilibanwa na Aston Villa ambao walitangulia kupata bao la mapema dakika ya 11 likifungwa na Jacky Grealish ambalo lilisawazishwa na Tom Heaton kwa kujifunga na victor Lindelof aliongeza bao la pili dakika ya 64 lililodumu kwa dakika 2 baada ya Tyrone Mings kusawazisha dakika ya 66.
Matokeo hayo yanaifanya United isalie nafasi ya 9 ikiwa na pointi 18 huku Arsenal waliotoka sare na Norwich wakisalia nafasi ya 8 na pointi 19.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.