Jana mashabiki wa klabu ya Yanga sc waliendeleza utamaduni wao wa kuwapokea mastaa wa timu hiyo wakimpokea mshambuliaji Saido Ntibanzokiza akitokea nchini Burundi kuja kujiunga na timu hiyo baada ya kusajiliwa wiki kadhaa nyuma.
Saido ni mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa akiwa amecheza vilabu kadhaa barani ulaya ikiwemo kucheza katika ligi ya Ufaransa hivyo wanayanga wana matumaini makubwa kwa staa huyo atamaliza ukame wa mabao klabuni hapo.
Mapokeza ya mchezaji huyo yaliongozwa na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Eng.Hersi Said akiwa na Mkuu wa Idara ya Habari Hassan Bumbuli pamoja naAfisa Hamasa Antonio Nugaz huku mashabiki wakijitokeza kama ilivyo kawaida yao
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.