Baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Pamba fc katika mchezo wa kirafiki jijini Mwanza baadhi ya mashabiki jijini humo wameoneshwa kutofurahishwa na matokeo hayo huku pia kiwango cha timu kwa ujumla kikionesha kutowafurahisha.
Mashabiki hao ambao walionekana kuwa na hasira baada ya mchezo kumalizika na walianza moja kwa moja kumlaumu kocha Zahera kutokana na kiwango kibovu cha timu hiyo hukun pia mshambuliaji David Molinga akionekana kutowafurahisha mashabiki.
Yanga imeweka kambi kanda ya ziwa kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Zesco Fc mchezo wa raundi ya kwanza baada ya kufanikiwa kuwatoa Township Rollers katika mchezo wa raundi ya awali,Mechi hiyo itafanyika septemba 14 jijini Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.