Wachezaji wa Arsenal, wamekubali kukatwa asilimia 12.5 ya mishahara yao, baada ya kuahidiwa ‘bonasi’ kubwa katika ligi ya mabingwa Ulaya na kombe la ligi ya Europa.
Wachezaji watafidia fedha watakazokatwa kwa kila mmoja kulipwa pauni laki moja (£100,000), endapo watafuzu kucheza msimu ujao wa ligi ya mabingwa ya Ulaya.
Klabu pia, imeahidi kumlipa kila mchezaji bonasi ya pauni laki tano (£500,000) kama watatwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2021 au pauni laki moja (£100,000) kama wataibuka mabingwa wa ligi ya Europa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Arsenal, imekuwa klabu ya kwanza ya ligi kuu England, kukubali mpango wa kukata mishahara kwa wachezaji wake, katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi duniani zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.