Home Soka Mastaa Simba sc Waoga Mamilioni

Mastaa Simba sc Waoga Mamilioni

by Sports Leo
0 comments

Bilionea kijana nchini, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ametoa mkwanja mrefu katika mechi ya jana Jumanne ambayo Simba ilikuwa nyumbani ikiibuka na ushindi wa mnono wa mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan.

Mo Dewji aliweka Dola za Marekani 100,000 ambazo ni zaidi ya Sh230 milioni. Pesa hizo ilikuwa kwa ajili ya kuongeza morali na motisha kwa wachezaji kupambana ili kupata ushindi ambao umewapa alama tatu na kufikisha pointi 10 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa vinara wa kundi A.

Mkwanja huo ambao unatolewa kama motisha utagawanywa katika makundi matatu – wachezaji waliocheza watapata si chini ya Sh10 milioni, waliokuwa benchi si chini ya Sh5 milioni na waliokuwa jukwaani kifuta jasho.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited