Home Soka Mbappe Akaribishwa Mtibwa Sugar

Mbappe Akaribishwa Mtibwa Sugar

by Sports Leo
0 comments

Staa wa timu ya taifa ya vijana (Ngorongoro Heroes) Kelvin John “Mbappe” amepewa ofa ya kufanya mazoezi na timu ya soka ya Mtibwa Sugar ili kujiweka fiti wakati akisubiri kwenda barani ulaya ambapo anatarajiwa kujiunga na timu ya Krc Genk ifikapo januari mwakani.

Mbappe amepewa nafasi hiyo na kocha wa timu ya taifa ya vijana Zubery Katwila ambaye pia ni kocha wa timu ya Mtibwa sugar inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Ninamfahamu vizuri Kevin, ni kijana mwenye nidhamu na malengo. Ni tofauti kabisa na wachezaji wengine, nimezungumza naye nikamuuliza malengo yake katika soka akaniambia anataka kucheza Ulaya, hilo ni jambo jema kwa kijana wa umri wake kuwaza kwenda mbali zaidi“Alisema kocha huyo.

banner

Kocha huyo aliyeiwezesha Ngorongoro Heroes kuchukua kombe la chalenji kwa vijana baada ya kuwafunga kenya kwa 1-0 alisisitiza kumhitaji mcheza huyo katika timu hiyo ili kumpa uzoefu zaidi.

Kwa vile hana timu hapa nchini na sasa hivi anasubiri ripoti ya majaribio yake Ulaya, mimi namkaribisha Mtibwa Sugar aje afanye mazoezi na apate uzoefu“, alisisitiza.

Kelvin amekua na kiwango kizuri baada ya kuibuka mfungaji bora katika michuano ya chalenji iliyoisha wiki iliyopita nchini Uganda huku pia akichukua tuzo ya mchezaji bora.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited