Yule mbaya wa Simba aliyewaua katika mechi ya kimataifa dhidi ya Ud Songo Luis Jose Miqquisone ananyemelewa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo la hivi sasa.
Staa huyo aliacha kilio uwanja wa taifa baada kufunga bao liliitoa rasmi Simba kwenye michuano ya kimataifa hadi kusababisha imani ya viongozi na mashabiki wa klabu hiyo kwa kocha Patrick Aussems kupungua kwa kiasi kikubwa tayari yupo kwenye rada za jangwani na tayari mchakato wa kumtumia tiketi ya ndege umeanza.
Staa huyo ni mali ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini na kama rada zitaa sawa anaweza kutua Jangwani kama mchezaji huru baada ya kuonyesha nia ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Mamelods ambayo humtoa kwa mkopo mara kwa mara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.