Home Soka Metacha Aikoa Yanga Sc

Metacha Aikoa Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Kipa wa klabu ya Yanga sc Metacha Mnata ameiokoa klabu hiyo na kipigo cha kwanza katika ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kuokoa penati dakika za majeruhi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Namungo Fc.

Yanga ilitangulia kupata bao dakika ya 13n kupitia kwa Carlos Calinhos aliyefunga kwa kichwa krosi ya Kibwana Shomari lakini bao hilo lilidumu kwa dakika 3 tu ambapo Steven Sey alisawazisha dakika ya 16 kufuatia makosa ya Farid Mussa.

Bakari Mwamnyeto alimuangusha Shiza Kichuya dakika ya 91 ndipo mwamuzi akatoa penati iliyopigwa na Bigirimana Blaise aliyekosa baada ya Metacha Kuipangua.

banner

Yanga sc imefikisha alama 25 sawa na Azam Fc huku Simba sc ikiwa na alama 23 huku mchezo unaokuja unatarajiwa kubadili msimamo ukiwakutanisha Azam Fc dhidi ya Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited