Klabu ya soka ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na magoli kipa wake wawili Metacha Mnata na Mkenya Farouk Shikalo mara baada ya kumalizika kwa mikataba yao.
Makipa hao walijunga na Yanga mwaka 2019 na wamekua wakipishana mara kwa mara kulinda lango la wananchi na kuondoka kwao kunatokana na jana Yanga kutangaza usajili wa golikipa wa kimataifa wa Mali Djigui Diarra.
Meatacha hakuonekana tena uwanjani tangu aliposimamishwa kutokana na kuwatukana mashabiki wake huku Shikalo ameshindwa kuwashawishi mabosi wake kumpa mkataba mpya.