Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema sababu kubwa ya kutomtumia mshambuliaji wake Juma Balinya katika mchezo wa kimataifa wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika ni uzito wa mchezaji huyo kuongezeka.
Zahara amesisitiza kuwa mchezaji huyo aliongezeka kilo baada ya kumaliza ligi kuu nchini Uganda hivyo kuwa mzito uwanjani wakati anajiunga na wanajangwani hao.
“Nilimtaka apunguze kilo haraka, nimpongeze kwenye hilo na tatizo ndiyo sababu ya kwanza kumuweka benchi mchezo wetu na Zesco tuliocheza hapa nyumbani licha ya kuwa na mipango ya kutaka kumtumia kwenye mchezo wa marudiano,” amesema Zahera.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo kocha huyo amesisitiza kuwa atamtumia mchezaji huyo kwenye mechi ya marudiano ugenini dhidi ya Zesco mchezo ambao Yanga inatakiwa ishinde au itoe sare kuanzia mabao 2.