Kiungo wa Simba sc Jonas Mkude ameingia matatani baada ya kuchelewa kuripoti kambini baada ya kupewa ruhusu hivyo kuchelewa ndege kwenda kanda ya ziwa ambapo timu hiyo ilikwenda kucheza michezo ya ligi kuu dhidi ya Kagera sugar na Biashara United.
Mkude alipewa ruhusa na uongozi ya kutoka kambini baada ya kuomba ruhusa kutatua matatizo ya kifamilia na alitakiwa kuwahi kuripoti kambini ili kujiunga na wenzake katika safari hiyo ambapo timu hiyo ilitumia usafiri wa ndege.
Ripoti kutoka katika klabu hiyo zinadai mchezaji alichelewa kuripoti na kuachwa na ndege huku pombe ikitajwa kusababisha mchezaji huyo kuchelewa baada ya kushindwa kuamka mapema na kupelekea kukosa michezo yote ya kanda ya ziwa ambapo timu hiyo ilifanikiwa kushinda.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Inasemekana suala hilo halijampendeza mtendaji mkuu wa timu hiyo Senzo Mazingiza ambaye aliagiza mchezaji huyo kusimamishwa na kusubiria hatua za nidhamu ambapo anaweza kukatwa mshahara ama kunyimwa posho ambazo watapata wachezaji wengine.