Pamoja na kukubali matokeo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi kuu, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema ratiba imechangia timu yake kutofanya vizuri leo
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, Mkwasa amelalamika kuwa ratiba haikuwa rafiki kwao
“Tumecheza Ijumaa Mwanza halafu Jumatatu tunacheza Dar es salaam. Wachezaji wangu leo hawakuwa katika ubora wao kutokana na uchovu,” amesema
“Hata hivyo nawapongeza KMC kwa kutupa changamoto, wamecheza vizuri”
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mkwasa amesema bado timu yake ina changamoto hasa katika safu ya ushambuliaji, amesema watatumia dirisha dogo kurekebisha tatizo hilo
“Bado tuna kazi ya kufanya, safu yetu ya ushambuliaji bado inashindwa kutumia nafasi nyingi tunazotengeneza. Kuelekea dirisha dogo nadhani tutakuwa na nafasi ya kufanya maboresho.