Home Soka Mkwasa Awatia Upepo Mastaa Yanga sc

Mkwasa Awatia Upepo Mastaa Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa muda wa timu ya Yanga sc Bonifasi Mkwasa ameanza rasmi kuifundisha klabu hiyo akichukua nafasi ya kocha Mwinyi Zahera ambaye amesitishiwa mkataba wake na uongozi wa klabu hiyo.

Mkwasa aliyekua katibu mkuu wa klabu hiyo kabla ya kujiengua kutokana na sababu za kiafya ameanza kazi rasmi kuiandaa timu hiyo dhidi ya mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda mkoani Mtwara.

Kocha huyo wa zamani wa Taifa stars amewahakikishia ushirikiano wachezaji wa timu hiyo ili kuleta furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo ambaye ilipitia kipindi kigumu hasa msimu uliopita ambapo ilikua na changamoto ya fedha.

banner

” Mpo hapa kuipigania klabu hii na kubeba vikombe, hilo ndo lengo la kwanza kwa kila mchezaji anayeitumikia klabu hii . . tunapaswa kuishi katika utamaduni huu na ili kutimiza dhamira hii ni lazima tuanze kushinda michezo yetu. . tutakaposhinda kila kitu kitarejea katika hali yake. . uwanja utajaa na furaha kwa mashabiki itarejea. . Nyie ni wachezaji wazuri sana nami nipo hapa kuwasaidia kufanikisha yote hayo”

Mkwasa akisaidiwa na kocha wa timu ya vijana ya klabu hiyo Said Maulid wanatarajiwa kuiongoza timu hiyo kwa kipindi cha wiki mbili wakati klabu hiyo ikitafuta kocha mpya kurithi nafasi ya Zahera.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited