Straika wa klabu ya Yanga David Molinga ameibuka shujaa katika mchezo dhidi ya Namungo Fc baada ya kusawazisha mabao mawili na kuifanya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 katika mchezo wa ligi kuu uwanja wa Taifa.
Awali Namungo walitangulia kupitia mabao ya Charles Edward aliyofunga dakika za 51 na 69 lakini kuingia kwa David Molinga kipindi cha pili kulibadili hali ya hewa baada ya kufunga mabao ya kusawazisha dakika za 79 na 95 na kufanya mchezo kumalizika kwa sare.
Yanga wamesalia nafasi ya tatu huku Namungo wakibaki nafasi ya nne ambapo Simba anaongoza ligi kwa jumla ya pointi 81 huku Azam fc ambaye alipoteza mbele ya Kagera Sugar akibaki nafasi ya pili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.