Pamoja na kusuasua kwenye kuzifumania nyavu katika michezo ya hivi karibuni, mshambuliaji wa Yanga David Molinga amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akiwahakikishia kuwa atauwasha moto mechi ijao
Jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union, Molinga alikosa mkwaju wa penati jambo lililowakera mashabiki wakati huo timu yao ikiwa nyuma kwa bao 1-0
“Ndio uhalisia wa mpira, kuna kufanya vizuri muda mwingine vibaya, leo sikuweza kufunga lakini nimepambana kuchangia ushindi,” alisema Molinga baada ya mchezo jana
“Nina amini mchezo ujao nitarejea kwa kishindo na kuweza kufunga ama kuisadia kushinda timu yangu, imekuwa siku mbaya kwangu kwa kutokufunga”
Inaelezwa Kaimu kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewapa mtihani washambuliaji Juma Balinya, David Molinga na Sadney Urikhob kuonyesha ubora wao ili waendelee kubaki kikosini
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga inatarajiwa kuongeza mshambuliaji dirisha dogo ambapo Ditram Nchimbi anatajwa kuja kuchukua nafasi huku Pengine kati ya washambuliaji waliopo jangwani mmoja anaweza kupewa mkono wa kwaheri.
Molinga ameifungia Yanga mabao mawili kwenye ligi yote akiyafunga mechi dhidi ya Polisi Tanzania.