Home Soka Molinga,Sadney Ndani Kuivaa Mbao

Molinga,Sadney Ndani Kuivaa Mbao

by Dennis Msotwa
0 comments

Mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga sc leo inashuka dimbani katika uwanja wa Ccm Kirumba kuvaana na mbao katika mchezo wa ligi kuu nchini ambapo kocha mwinyi Zahera tayari ametoa orodha ya wachezaji watakaoanza.

Katika nafasi ya golini Farouk Shikalo atasimama badala ya Metacha Mnata huku safu ya ulinzi ikiwa ni Juma Abdul,Ally Sonso,Ally Ally na Kelvin Yondan na eneo la kiungo litakua na Feisal Salum,Papy Tshishimbi,Mrisho Ngasa na Mapnduzi Balama wakati David Molinga na Sadney Urikhob wataongoza safu ya ushambuliaji.

Wachezaji Mybin Kalengo,Gustapha Simon,Ramadhani Kabwili,Patrick Sibomana,Rafael Daud,Abdulazizi Makame na Juma Balinya watakua benchi katika mchezo huo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited