Unaweza kusema ni kufuru,Baada ya mshambuliaji wa Simba sc mwenye asili ya Kinywaranda Meddie Kagere kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni msimbazi baada ya ule wa awali kusalia msimu mmoja pekee.
Mchezaji huyo aliyekua anawaniwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Afrika ikiwemo Zamalek ya Misri,Tp Mazembe ya Kongo amesaini mkataba mpya na wanamsimbazi hao na kuzima tetesi za muda mrefu za kuondoka klabuni hapo huku ikidaiwa Zamalek wameweka dau la shilingi bilioni moja ili kumnasa.
Taarifa za ndani zinasema Kagere atapokea mshahara mara mbili ya ule wa awali unaokadiriwa kufikia shilingi milioni 12 za kitanzania aliokuwa akipokea tokea ajiunge na wekundu hao akitokea Gormahia Fc ya Kenya na hivyo kwa makadirio mshahara mpya wa mshambualiaji huyo unazidi kiasi cha shilingi milioni 20 kwa mwezi ambapo mshahara huo ukiugawa kwa wiki unazidi shilingi milioni 5.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba imeshawishika kuvunja benki ili kumbakiza mshambuliaji huyo mwenye nguvu baada ya kuwa na msimu mzuri wa ligi kuu bara akiibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 23 katika mechi 36 za ligi kuu bara.