Home Soka Mshahara wa Kagere Kufuru Simba

Mshahara wa Kagere Kufuru Simba

by Dennis Msotwa
0 comments

Unaweza kusema ni kufuru,Baada ya mshambuliaji wa Simba sc mwenye asili ya Kinywaranda Meddie Kagere kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni msimbazi baada ya ule wa awali kusalia msimu mmoja pekee.

Mchezaji huyo aliyekua anawaniwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Afrika ikiwemo Zamalek ya Misri,Tp Mazembe ya Kongo amesaini mkataba mpya na wanamsimbazi hao na kuzima tetesi za muda mrefu za kuondoka klabuni hapo huku ikidaiwa Zamalek wameweka dau la shilingi bilioni moja ili kumnasa.

Taarifa za ndani zinasema Kagere atapokea mshahara mara mbili ya ule wa awali  unaokadiriwa kufikia shilingi milioni 12 za kitanzania aliokuwa akipokea tokea ajiunge na wekundu hao akitokea Gormahia Fc ya Kenya na hivyo kwa makadirio mshahara mpya wa mshambualiaji huyo unazidi kiasi cha shilingi milioni 20 kwa mwezi ambapo mshahara huo ukiugawa kwa wiki unazidi shilingi milioni 5.

banner

Simba imeshawishika kuvunja benki ili kumbakiza mshambuliaji huyo mwenye nguvu baada ya kuwa na msimu mzuri wa ligi kuu bara akiibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 23 katika mechi 36 za ligi kuu bara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited