Home Soka Mudathir Aiokoa Yanga sc

Mudathir Aiokoa Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Bao pekee la Mudathir Yahaya Abbas limeipa alama tatu Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam dhidi ya Dodoma Jiji Fc na kuipaisha timu hiyo katika msimamo wa ligi kuu nchini.

Yanga sc ilibidi ifanye kazi ya ziada kutokana na uimara wa Dodoma Jiji kuokoa hatari wakiongozwa na Joram Mgeveke na Mtenje Albano waliokua hatari kwa Yanga sc muda wote wa  mchezo huo ambao ulikua wa kasi muda wote.

Ikianza na washambuliaji Kennedy Musonda na Joseph Guede Yanga sc ilitengeneza nafasi za kufunga lakini umakini ulikua mdogo kwa washambuliaji hao ambapo ilimlazimu kocha kumuingiza Clement Mzize kipindi cha pili pamoja na Mudathir aliyechukua nafasi ya Jonas Mkude.

banner

Pasi nzuri ya Pacome Zouzou ilimkuta Nickson Kibabage  aliyepiga pasi nzuri kwa Mudathir aliyefunga bao hilo lililoamsha shangwe kwa mashabiki na viongozi wa Yanga sc dakika ya 86 ya mchezo huo na mpaka dakika tisini zinakamilika Yanga sc waliondoka na furaha ya ushindi huo.

Sasa Yanga sc wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc wakiwa na alama 34 katika michezo 13  huku Azam Fc wakiwa katika nafasi ya pili na alama 31 na Simba sc wakiwa nafasi ya tatu na alama 26 katika michezo 11 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited