Home Soka Namungo FC wafanya utalii

Namungo FC wafanya utalii

by Sports Leo
0 comments

Klaby ya Namungo ya Lindi imefanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi ya taifa ya Bonde la Ngorongoro iliyopo Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya burudani na kuchangamsha na kuweka akili sawa kueleka msimu mpya ligi kuu soka Bara.

Wauaji hao wa Kusini wameweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/2022 katika akademi ya soka ya Black Rhino iliyopo katika Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Mastaa mbalimbali wa timu hiyo wameonekana wakifurahia ziara hivyo,wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha la usajili kama David Molinga na Obrey Chirwa walionekana wakichukua picha mbalimbali za ukumbusho hifadhini hapo.

banner

Namungo inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa msimu wa 2021/2022 Septemba 27 dhidi ya Geita Gold katika dimba la Ilulu watakalolitumia kipindi ambacho uwanja wake wa nyumbani wa Majaliwa ukiwa katika marekebisho pamoja na ufungaji wa taa.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited