Timu ya Mtibwa Sugar imesajili wachezaji Said Mohamed “nduda” na Salim Mbonde waliotemwa na klabu ya Simba baada ya miaka miwili kupita tangu waondoke klabuni hapo kwenda kujiunga na Wanamsimbazi.
Nduda ambaye amewahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma alisajiliwa na Simba baada ya kuonesha uwezo akiwa na mtibwa sugar lakini alishindwa kufua dafu mbele ya Aishi Manula na Deo Munishi huku ikichangiwa na majeruhi ya goti yalimfanya akatibiwe nchini India na baadae alitolewa kwa mkopo kwenda Ndanda ya mtwara.

Salim Mbonde
Kwa upande wa Mbonde ni kama hakuwa na bahati na Simba baada ya kuumia na kukaa muda mrefu akiwa majeruhi hadi hapo alipokubaliana na Simba kuvunja mkataba kwa maslahi ya pande mbili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msemaji wa Mtibwa Thobias Kifaru alithibitisha kuwasajili wachezaji hao na kusisitiza kwamba wamerudi nyumbani.