Kiungo fundi wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima ataukosa mchezo wa leo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika katika uwanja wa Majaliwa mkoani Mtwara.
Kiungo huyo ataukosa mchezo huo baada ya kuwa na kadi tatu za njano alizopata katika mechi za ligi kuu hivyo kwa mujibu wa kanuni ataukosa mchezo huo kama adhabu.
Wengine watakaokosa mchezo huo ni Kelvin Yondani mwenye matatizo ya kifamilia huku Adeyun Salehe na Mohamed Issa Banka ataukosa kutokana na kuwa majeruhi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.