Kocha Cedrick Kaze amethibitisha kuwa kiungo mkongwe Haruna Niyonzima na Carlos Carlinhos ni miongoni mwa mastaa wa klabu ya Yanga sc watakaoikosa derby ya Dar es salaam baina ya Yanga sc na Simba sc.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo mkubwa nchini Kaze alisema kuwa wachezaji hao walipata majeraha huku Carlinhos akisumbuliwa na enka na Niyonzima akisumbuliwa na Maralia.
Licha ya kuanza mazoezi siku kadhaa zilizopita kocha Kaze amedai wachezaji hao wanakosa utimamu wa mwili kuweza kushiriki mchezo huo.