Staa mpya wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza ameendelea kudhihirisha ubora wake baada ya kuisaidia timu ya Taifa ya Burundi kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mauritania katika kuwania kufuzu Afcon mwaka 2021.
Saido licha kuisaidia Burundi kuondoka na alama moja katika mchezo wa Awali nchini Mauritania ambapo alisawazisha bao kwa faulo na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 huku akifanya maajabu katika mchezo pili nchini Burundi kwa kufunga mabao mawili katika ushindi huo wa 3-1.
Saido ni mchezaji aliyesajiliwa na Yanga sc na ataanza kuitumikia timu wakati wa dirisha dogo huku akitarajiwa kuanza mazoezi muda si mrefu baada ya kumaliza michuano ya kimataifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.