Home Soka Okwi Amuua Zahera

Okwi Amuua Zahera

by Sports Leo
0 comments

Mganda Emmanuel Okwi amesaidia timu yake ya taifa kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Kongo inayonolewa na kocha wa Yanga sc Mwinyi Zahera ambaye anamsaidia Frolent Ibenge ambaye ni kocha mkuu wa timu hiyo.

Uganda walionyesha kujiamini toka mwanzo wa mchezo na kufanikiwa kufanya mashambulizi kadhaa na iliwachukua dakika 14 za kipindi cha kwanza kupata goli la ufunguzi lililofungwa na Patrick Kaddu mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea timu ya Kcca ya nchini kwao Uganda.

The Cranes waliendelea kulishambulia lango la wakongo na hatimaye muuaji Emmanuel Okwi alifanikiwa kuipa Uganda bao la pili dakika ya 48 baada ya kutoka mapumziko.

banner

Kwa ushindi huo Uganda imekaa kileleni mwa kundi A wakifuatiwa na wenyeji Misri  huku Zimbabwe akishika nafasi ya tatu na Kongo wakiwa mkiani mwa kundi hilo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited