Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba sc Emmanuel Okwi amekumbwa na ukame wa mabao baada ya kucheza mechi tatu za ligi kuu nchini Misri na kushindwa kufunga bao.
Okwi anayeichezea klabu ya Al Ittihad ya nchini humo mpaka sasa amecheza mechi hizo huku mbili akimaliza dakika 90 na moja akicheza kwa dakika 65 lakini hajafunga mpaka sasa kinyume na matarajio ya wengi baada ya kufanya vizuri akiwa nchini.
Okwi alicheza dhidi ya Zamalek na El Gouna kwa dakika zote tisini na hakufunga bao licha ya timu yake kupoteza kwa bao 1-0 huku mechi dhidi ya Al Masry wakishinda kwa bao moja huku wakishika nafasi ya tano kwenye ligi baada ya kuwa na pointi 6 huku Al Ahly wakiongoza ligi kwa pointi 9.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.