Home Soka Panga Zito Jangwani

Panga Zito Jangwani

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuwa upo kwenye mipango madhubuti ya kufanya usajili mkubwa katika dirisha la usajili la mwezi Juni mwaka huu kwa kuleta majembe mapya ya kazi, na kuwaondoa baadhi ya nyota ambao wanaonekana kuwa na mchango mdogo kwenye kikosi hicho.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Yanga ambao inatajwa wapo kwenye hatari ya kuachwa ndani ya kikosi hicho ni washambuliaji Michael Sarpong, Fiston Abdoul Razak na Ditram Nchimbi ambao kwa jumla wao wamefunga mabao sita tu kwenye ligi mpaka sasa.

Katika siku za hivi karibuni Yanga wameonekana kukosa makali, hasa katika safu yake ya ushambuliaji ambapo licha ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 51, kikosi hicho kimepata ushindi mmoja pekee kati ya michezo saba iliyopita imefungwa mechi moja na kutoa sare michezo mitano.

banner

Cc:Gpl

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited